Google — Year In Search 2021

Google — Year In Search 2021

SUBTITLE'S INFO:

Language: Kiswahili

Type: Human

Number of phrases: 51

Number of words: 411

Number of symbols: 2692

DOWNLOAD SUBTITLES:

DOWNLOAD AUDIO AND VIDEO:

SUBTITLES:

Subtitles prepared by human
00:00
["Mwaka huu kuliko mwaka mwingine wowote"] [sauti ya kinanda inasikika] [“Mwaka huu kuliko mwaka mwingine wowote ulimwengu ulitafuta”] [mwanamke anazungumza kwa uchovu] Nimekumbwa na changamoto nyingi katika mwaka huu. [“jinsi ya kupona” kwa Kihispania] [“jinsi ya kupona” kwa kiindonesia] [“jinsi ya kupona” kwa Kirusi] Nimetamaushwa. [“jinsi ya kupona”] [“kupona”] Na ninapona. [“jinsi ya kumheshimu mtu”] [sauti ya mwanamke Mwingereza] Niko hapa kwenye ukuta wa makumbusho. [“jinsi ya kuheshimu mtu”] Nilitaka kufanya kitu ili kumkumbuka mama yangu. ["je kutakuwa na kufungwa tena"] [mwanamke anaongea] Kwa sababu fulani nina, wasiwasi. Kwa dhahiri ni kawaida na kwa kila kitu ambacho kinaendelea sasa. [“jinsi ya kutunza afya yako ya akili”] [Naomi Osaka anazungumza] Nadhani nitapumzika kwa muda. [Isaac Frère anazungumza] Unaweza kukabili hali hii. Na ikiwa unaweza kuikabili, [“jinsi ya kustahimili”] kuna thawabu kubwa upande ule mwingine. [“ninaweza kupata chanjo lini”] [sauti ya mwanaume] Kama wanavyopokea watu wengine, Ninajaribu kuwajibika ili nijaribu kuokoa jumuiya yangu. [sauti ya mwanamke] Ta-da! ["jinsi ya kuwa mtahimilivu"] [saiti ya mwanamume] Nimefurahia sana kuwa imefunguliwa tena. Na bado ninaendelea kutabasamu chini ya barakoa yangu! [sauti ya mtangazaji wa spoti] Matukio bora zaidi ya siku [“jinsi ya kurudi”] mashabiki walirudi. [Lin-Manuel Miranda anazungumza] Karibuni tena kwenye ukumbi! [umati unashangilia] [Billie Eilish anazungumza] Watu wangu, imekuwa muda mrefu sana! [umati unashangilia] [“jinsi ya kuwa wewe mwenyewe”] [Elliot Page anazungumza] Unajitazama kwenye kioo, na kujiambia, “Huyu. Ni. Mimi.” [“kusudi langu ni lipi”] [Michael K. Williams anazungumza] Kuwa mtu bora zaidi. Kamwe, usiwahi kukosa kuwa na maono.
01:06
Sijali wanachokuambia. [hadhira inashangilia] [sauti ya muziki inarudi chini na kutulia] [Hakimu Peter A. Cahill anazugumza] ...sisi wanajopo katika hali iliyobainishwa hapo juu ["jinsi ya kusonga mbele"] kama kuhesabu moja hadi tatu tunampata mshtakiwa kuwa na hatia. [“drivers license” ya Olivia Rodrigo inasikika] [“tupinge chuki dhidi ya waasia”] [Sandra Oh anazungumza] Najivunia kuwa Mwasia. [umati unashangilia] ["jinsi ya kutumia sauti yangu"] [Brianna Fruean anazungumza] Hatuzami, tunapigana. [“jinsi ya kusaidia sayari yetu”] [Vanessa Nakate anazungumza] Hatuwezi kunyamaza huku uchafuzi wa mazingira ukiendelea. Hakuna hatua ndogo mno. ["njia ya kusaidia jamii yako"] [sauti ya mwanamume] Ni muhimu tujiunge pamoja kama jamii, na kurudisha maisha ya watu. [“nitatembelea familia yangu lini”] [anazungumza huku akitokwa na machozi] Mwanangu. [akicheka na kutokwa na machozi ya furaha] [Amanda Gorman anazungumza] Kwamba licha ya kuwa na huzuni, tulikua. [“jinsi ya kuwa na matumaini”] Kuwa licha ya kuumwa, tulitumaini. Licha ya kuwa tumechoka, tulijaribu. Kuwa daima tutakuwa pamoja, tutashinda. [“Kwa kila mtu anayejitahidi kuinuka tena”] [muziki unaanza kufifia kwa upole] [“Endelea kutafuta.”] [muziki unafifia polepole]

DOWNLOAD SUBTITLES: